Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akifanya usafi maeneo ya soko la sabasaba Mkoa wa Mwanza katika kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella anawakaribisha wakazi wote wa Mwanza,kanda ya ziwa Magharibi na maeneo ya jirani kwenye maonyesho ya nanenane yatakayofanyika Uwanja wa Nyamuhongolo uliopo Mkoa wa Mwanza.
Serikali Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza imekemea tabia za wazazi na walezi wanaolazimisha watoto wa kike kufeli mitihani yao ya elimu ya msingi ili wawaozeshe kwa nia ya kupata mahari.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wazazi na walezi watakaobainika kuwaozesha wanafunzi kwa nia ya kupata mahari pamoja na wale wanaokatisha ndoto zao za kitaaluma kwa kuwapa ujauzito.
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.